Logo

Habari mambo-leo hapa MMBongo

Habari
18 Juni 2018
Habari za Sanaa na ulimwengu wa burudani kila wiki hapa MMBongo! Karibuni, tumewaandalia burudani ya kipekee, hauna haja ya kutoka nyumbani! SOMA ZAIDI!
<p>Screen Shot 2018-05-31 at 16.26.10</p>

Habari za Sanaa na ulimwengu wa burudani kila wiki hapa MMBongo! Karibuni, tumewaandalia burudani ya kipekee, hauna haja ya kutoka nyumbani!

Tukilenga macho kwenye vipindi vyetu vya MMBongo, msimu wa tatu wa HUBA umefikia kikomo kwenye kilele cha uhondo! Ushuhuda mpya alioupata Tima utasababisha awachiliwe huru? Jude naye amejifunga pingu za mahusiano na wanawake wawili, huku ikileta kasheshe katika maendelezo ya kibiashara. Batuli na Kibibi jino kwa jino kushinda penzi lake ili kumtumia kupata matakwa yao katika Fuli Gem Stones.

Kweli, Maisha ni panda-shuka jamani, tukiangalia jinsi Maisha ya Samrat yamebadilika! Urmi naye anaendelea kupambana na Mama Mkwe mpya ambaye anamchukia kupindukia. Penzi lake na Ishaan litadumu? Tunaendelea kuelimika sana kuhusu mada ya mahusiano ya kijamii haswa katika jumuiya ya kihindi! Mwana wa kike huwa anapambana na changamoto nyingi kuanzia msimamo wake katika familia, swala la elimu na mavazi, maswala ya ndoa na uhuru wa kuchagua mpenzi wake, kisha, Maisha katika familia ya mashemeji. Katika tamthilia ya Doli Armano Ki, swala la Haki za Wanawake linasimamia pande gani?

Wasanii wakongwe wa Bongo Fleva wanawahimiza wasanii wa kisasa kutilia maanani uandishi na uzalishaji wa muziki bora unaovuka mipaka kote duniani badala ya kuleta uvumi na kiherehere katika sekta ya burudani. It is all about the music!