Logo

Hongera kwa Wanaharakati walioteuliwa na Avance Media 2017

Habari
29 Decemba 2017
Wanaharakati walioteuliwa katika uchaguzi wa wanatanzania 50 waliofuzu katika sekta tofauti na Avance media wametangazwa!
Jokate-mwegelo

 

Wanaharakati walioteuliwa katika uchaguzi wa wanatanzania 50 waliofuzu katika sekta tofauti na Avance media wametangazwa!

Tungependa kuwapa pongenzi wasanii na wanasanaa ya filamu na televisheni walioteuliwa! Wengi wao wameshiriki katika vipindi na filamu zilizopeperushwa hapa Maisha Magic Bongo. Pata kuwajua wanaharakati wetu! 

Muigizaji, Jokate Mwegelo

Muigizaji na mmiliki wa Sio Habari. Idris Sultan ameigiza katika tamthilia ya Sarafu inayopeperushwa Januari 2018 hapa MMBongo!

Wasanii vikongwe wa Bongo fleva, Ali Kiba na Diamond Platnumz.

Muigizaji mashuhuri, Wema Sepetu

Muigizaji, Luca Mhuvile (Joti) mcheshi shupavu katika kipindi cha Mwantumu.

Msanii wa Bongo fleva, Vanessa Mdee

Muigizaji mashuhuri katika tamthilia yetu ya HUBA na mcheshi hodari katika sekta ya sanaa.

 

Sekta ya sanaa na burudani inaendelea kuimarika hapa Tanzania, wasanii na waigizaji wetu wakiendelea kupata umaarufu kote duniani! Tunawashukuru sana kwa kazi yenu na pongezi kwa kupata fursa ya kuwa katika Orodha hii ya Avance Media 50 Most Influential Young Tanzanians!