Logo
Mengine Zaidi
channel logo dark

Pazia

160TamthiliaPG13

Kifo cha msanii mashuhuri 'Brah' Hugh Masekela

Habari
25 Januari 2018
Mwana Muziki mkongwe kutoka Afrika Kusini, Bwana Hugh Masekela aliaga dunia wiki hii nyumbani kwake, katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini.
 cover

Mpigaji tarumbeta mashuhuri na Mwana Muziki mkongwe kutoka Afrika Kusini, Bwana Hugh Masekela aliaga dunia wiki hii nyumbani kwake, katika jiji la Johannesburg, Afrika Kusini. Taarifa za kifo chake zilitolewa na familia yake kwa vyombo vya habari.  

Bwana Masekela aliyejulikana kama “Brah Hugh” alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Saratani tangu mwaka wa 2008.

Katika siku zake za usoni, Brah Hugh alifanikiwa kutembea katika bara la Afrika na kote duniani akieeneza wito wa Umoja na usawa. Alikua miongoni mwa watu waliopigania haki sawa na uongozi bora, haswa, Afrika Kusini iliokua chini ya serikali ya Apartheid. Muziki wa Brah Hugh unajulikana kote duniani, akiwa kama balozi wa tamaduni za KiAfrika katika nchi za ulaya. Alikuwa mmoja wa wasanii walioheshimika duniani kote. Alitumbuiza katika tafrija mbali mbali ikiwemo sherehe za AMVCA 2017 mwaka uliopita.

Pata video ya Hugh Masekela akiwa katika Sherehe za DSTVMCA 2017 HAPA

Brah Hugh Masekela alipata fursa kuongoza chama cha wanamuziki wa  ‘Jazz’ nchini mwake, Aliheshimiwa na kupendwa sana.

Daima mioyoni mwetu  Brah Hugh Masekela, Mungu ailaze moyo wake vyema peponi.