Logo

MultiChoice Yawekeza katika tasnia ya filamu Afrika

Habari
12 Juni 2018
Program ya MultiChoice Talent Factory kuuboresha ubunifu wa Watanzania! Wasilisha ombi lako kabla ya tarehe 5 Julai 2018!
MTF feature image

 

MultiChoice Africa, Imezindua rasmi program kubwa ya kijamii inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu hapa Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

 Program hiyo ijulikanayo kama MultiChoice Talent Factory (MTF) inalenga kuchochea ubunifu wa vijana wa Afrika katika tasnia ya filamu. Imeandaa vyuo maalum vitatu ambavyo vitatoa mafunzo maalum ya utengenezaji wa filamu kwa vijana kutoka nchi mbalimbali kote barani Afrika.

“Maendeleo ya nchi yetu kwa muda mrefu yamekuwa yakitambuliwa kwa uwekezaji katika maliasili nyingi tulizonazo kama vile madini, kilimo, mifugo, wanyamapori, na kadhalika, sekta ya ubunifu ikiwa haijapewa kipaumbele kikubwa na hivyo sekta ya sanaa na ubunifu kuwa na mchango mdogo katika ukuaji wa uchumi wetu. Ili kuhakikisha kuwa tunasaidiana na serikali katika mkakati wake wa kuifanya sekta ya ubunifu na sanaa kuwa moja ya mihimili ya uchumi wetu, MultiChoice imeanzisha program hii na tumeanza na sekta ya filamu” alisema Maharage Chande, Mkurugenzi wa MultiChoice kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Tumebarikiwa kwa vipaji vingi katika fani mbalimbali na bila shaka tukiwekeza katika vipaji vya vijana wetu. Bila shaka, tutafanikiwa kupanua wigo wa ajira na uchumi wetu na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu

Amesema Program hiyo, itakayoanza rasmi mwezi Oktoba mwaka huu, itawawezesha vijana wanne kutoka Tanzania kuungana na vijana wengine kutoka nchi mbali mbali za Afrika katika vyuo maalum vya mafunzo ya utengenezaji wa filamu, ambavyo vitakuwa nchini Nigeria, Kenya na Zambia.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harison Mwakyembe amesema program hiyo itakuwa chachu kubwa katika kuleta mapinduzi kwenye tasnia ya filamu hapa nchini kwani vijana watakaopatikana mbali na kwamba watakuwa na uwezo wa hali ya juu wa kutengeneza filamu, bali pia, watakuwa kama waalimu wa wezao ambao wanavipaji katika tasnia hiyo.

“Nimefurahi sana kusikia kuwa MultiChoice wanapanga kuendelea na mpango huu kwa muda mrefu kwa hiyo, japokuwa tunaaza kwa kupeleka wanafunzi wanne, bado tunaamini huu ni mwanzo mzuri sana. Cha msingi kwanza siyo idadi ya wanafunzi, bali ni umuhimu wa chuo hicho na kiwango cha mafuzo kitakachotolewa. Tunaamini kwa mwaka huu wa kwanza vijana hao wakikamilisha mafuzo yao na kurudi nyumbani, watakuwa chachu kubwa katika kukuza na kuimarisha tasnia ya filamu hapa nchini”.

Pia ametoa rai kwa MultiChoice kushirikiana kwa karibu na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na pia vyuo vyetu ambavyo vinatoa elimu ya sanaa ya filamu ili kuhakikisha kuwa wanabadilishana ujuzi na uzoefu. Ikiwezekana kuwa na miradi ya pamoja ya muda mrefu na mfupi na hivyo kuwafikia vijana wengi zaidi na kuweza kutimiza lengo kuu la kuifanya fani ya filamu kuwa moja ya nguzo za uchumi wa nchi hii.

Program hiyo inaanza rasmi kwa kupokea maombi ya washiriki ambayo yatapokewa kwa njia ya mtandao.

Kwa ufupi:

  • Programu hii inamruhusu mtanzania anayekidhi vigezo kuingia kwenye mashindano ya kupata washindi wanne ambao watadhaminiwa kwa mwaka mmoja kwa mafunzo yote yahusuyo utengenezaji filamu.
  • Maelezo zaidi yanapatikana kwenye tovuti ya www.multichoicetalentfactory.com
  • Vilevile, kutakuwa na namba maalum ambayo inapatikana kuanzia tarehe 1 June 2018.
  • Wanaotaka kushiriki wanaweza kuanza kuwasilisha maombi yao kuanzia sasa na mwisho ni tarehe 4 July 2018.
  • Hakuna gharama za kushiriki kwenye mashindano.
  • Mafuzo rasmi kuanza mwezi wa Oktoba 2018, jijini Nairobi, Kenya.
  • Washindi watakaochaguliwa watakuwa wanne (4)
  • Gharama zote zitalipiwa na Multichoice kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Jiunge na ulingo wa MTF Mitandaoni kwa  #multichoicetalentfactory kisha fuata au jiunge kwa:

  •  Instagram: @multichoicetalentfactory
  • Twitter: @MCTalentFactory
  • Facebook: @multichoiceafricatalentfactory

 

Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:

Johnson Mshana

Mkuu wa Mawasiliano

[email protected]