Logo
channel logo dark

Kumi Za Wiki

160Muziki13

Rayvanny anateuliwa katika BET Awards na kushiriki katika Coke Studio Africa!

Habari
26 Juni 2017
Tazama MZOOKA Jumatatu hadi Ijumaa saa 10 jioni
Rayvanny anateuliwa katika BET Awards na kushiriki katika Coke Studio Africa! Image : 76

Mwana Muziki maarufu kutoka Tanzania, RayVanny anapeperuka mwaka huu! Anajulikana kuwa msanii aliyepaa kama Staa bora wa muziki hapa Afrika Mashariki. Nyota wa Afrika Mashariki wa Kipekee, aliteuliwa katika shindano la International Viewer’s Choice Awards (2017) na BET Awards 2017. Isitoshe, akishirikiana na DjTafinha kutoka Angola, ameshiriki katika Coke Studio Africa kwa mara yake ya kwanza, mwaka huu! RayVanny ni mmoja kati ya  wasanii wanaoshiriki katika kipindi cha ‘The Global Fusion Edition’ katika mtandao wa Coke Studio Africa pamoja na msanii kutoka Marekani Jason Derulo na wanamuziki wengine wengi kutoka  Afrika.

 

Wasanii hawa ni Dela(Kenya), Bebe Cool (Uganda), Mr. Bow (Mozambique), Falz (Nigeria), Joey B (Ghana), Betty G (Ethiopia), Jah Prayazah (Zimbabwe), Shekhinah (South Africa), Locko (Cameroon) and Denise (Madagascar).

 

Akizungumza katika mahojiano yaliofanyika The Stanley Hotel mjini Nairobi, RayVanny alisema, “Uhusiano wangu na Coke Studio na kazi tuliyofanya na wasanii wenzangu Jason Derulo umenimarisha sana katika muziki wangu. Tumerekodi nyimbo kadhaa  mashabiki wetu wategemee mengi zaidi! Nina furaha kweli kuwa hapa kwani ilikuwa ni miongoni mwa ndoto zangu kufika hapa. Shukrani sana kwa Coke Studio Africa, muziki unatuunganisha.”

 

Coke Studio Africa ni kongamano la muziki kutoka maeneo yote ya bara la Afrika. Kipindi hiki hakina lengo la mashindano. Haswa, lengo lao ni kuileta Afrika pamoja kwa kutumia burudani ya muziki kutoka kote Afrika. Inawaunganisha wasanii tofauti walio na mitindo tofauti tofauti ya muziki na sanaa kuzalisha mtindo wa ukoo wetu wa KiAfrika.

 

Maproducer wawili kutoka Afrika: DJ Maphorisa (Afrika Kusini) na Masterkrft (Nigeria) ndio waandaji wakuu wa Coke Studio Afrika . Msimu mpya wa Coke Studio Africa kuanzia Septemba.

 

Rayvanny ni msanii wa pekee aliyeteuliwa kutoka Afrika Mashariki katika shindano la BET Awards litakalokuwa tarehe 25 Juni 2017 katika Ukumbi wa Microsoft, mjini Los Angeles, nchi ya Marekani. Rayvanny alikuwa na haya ya kusema, “Nina nia ya kuboresha na kuwafurahisha mashabiki wangu. Nimeteuliwa kuwa msanii bora kutoka Afrika Mashariki katika shindano la BET Awards mwaka huu. Ninawaomba supoti yenu kwa kunipigia kura katika hashtag #IpickRayvanny katika The 2017 BET Awards.”

 

Sherehe ya BET Awards ina lengo la kutambua na kuwapa mkono au tuzo wasanii waliomeremeta katika sekta za Burudani, haswa, kuhusiana na Ubora wa Muziki.

Rayvanny anajulikana kwa nyimbo zake Zezeta, Kwetu, Natafuta Kiki na Salome.

 

Je, tuzo la BET Awards litakuja Afrika Mashariki? Tuwasapoti wasanii wetu kwa kupiga kura katika mitandao ya social media. Hashtag ni: #IpickRayvanny

Tazama video za RayVanny katika kipindi cha MZOOKA, kila Jumatatu hadi Ijumaa saa 10 jioni kupitia DStv chaneli 160!

 

Kupata habari zaidi, temebelea kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na tovuti yetu: maishamagicbongo.tv