Logo

Wahusika katika HUBA msimu wa Tatu!

Habari
31 Mei 2018
Tumekaribia chanzo cha msimu wa tatu hapa #HUBATZ! Je, unawakumbuka wahusika wa tamthilia hii? Unawajua waigizaji wapya? Soma zaidi!
HUBa article cover

Siku zinasonga na muda unayoyoma! Ngoja ngoja huumiza matumbo, lakini, subira pia huvuta heri! Hivyo basi, kabla hatujawaandalia yaliyojiri katika msimu mpya wa HUBA, pata kuwajua wahusika! 

JUDE

Bena Kinyaia anajulikana kama Jude ni muhusika mgeni katika tamthilia hii. Ni muigizaji na ni presenter wa vipindi mbali mbali kwenye Runinga.

Ni mara yake ya kwanza kuwa katika cast ya HUBA akicheza kama bossi mpya katika kampuni ya Fuli Gem Stones baada ya Dev kuondoka kwa ghafla. Anakabiliwa na jukumu sio la kuendesha kampuni pekee, bali, pia la kukabiliana na wanasiasa wa ofisi wakiwemo Jojo, Kibibi na Batuli.

 

TIMA

Kidoa Salum ajulikanaye kama Tima ni mke na mama-mtoto wa Dev. Ni binti ya Kashaulo na Mgeni. Tima  anapambana na adui wa wengi, wakiwa wanawake wa kampuni ya Fuli Gem Stones, sababu kubwa ikiwa wivu wa mapenzi. Ndoa imepitia changamoto nyingi kwa ajili ya hawa wanawake!

Msimu uliopita alikumbwa na janga kubwa iliyoweka matatani. Katika msimu huu, binti Kashaulo yupo gerezani akitumikia kifungo chake kutokana na mashtaka yanayomkabili, huku mama yake na baba yake wakifanya juu chini kumsaidia.  Baba mtoto wake Dev naye amepotelea mbali, haonekani.

HUBA inaanza tarehe 4 Juni, saa 3 usiku. Usikose kipindi cha kwanza!