Logo

Wiki hii hapa MMBongo!

Habari
23 Julai 2018
Vipindi vipya na habari za kisasa hapa #MMBongo! Je, tumewaandalia nini? SOMA ZAIDI!
<p>Screen Shot 2018-07-23 at 12.42.10</p>

HARUSI YETU MSIMU WA TATU:

Kuanzia Alhamisi iliyopita, msimu wa tatu wa Harusi Yetu ulirudi hewani! Harusi ya kwanza msimu huu ilikuwa ndoa kati ya Magareth na Solomon ambao walikuwa washindi wa shindano la msimu uliopita. Maisha Magic Bongo na MNET waligharamia harusi nzima na safari ya Honeymoon na sherehe ilikuwa ya kukata na shoka! Wiki hii, tunapata kusafiri na wanandoa wengine katika matayarisho yao! Usikose kuungana nasi, Kila Alhamisi saa 1 usiku, kipindi ni #HarusiYetuTZ Pata picha za harusi yao katika hii linki: https://bit.ly/2NDgH1g

 

BLOOD:

Tamthilia mpya hapa MMBongo inaelekea kipindi cha tatu Jumanne ijayo! Stacy anapogundua ameathiriwa ugonjwa wa Ukimwi,  anaamua kumtafuta aliyemshikisha maradhi haya, huku akikimbizana na wanaume aliotoka na wao zamani. Heka heka zikiendelea, Mume wake Tony anakiri jambo la kustaajabisha! Ungana nasi kila Jumanne ne Jumatano saa 1.30 usiku kufuatilia uhondo huu!

 

HUBA MSIMU WA TATU: 

Wakati Jude na Roy waliteuliwa kuwa wakurugenzi wasimamizi katika Fuli Gem Stones, Wanawake katika kampuni wamejitahidi kujipendekeza kwao ili kutimiza matumaini yao ya ki-biashara. Dev anarudi kighafla na pia Tesa ako na wasiwasi matumaini yake ya kuwa mkurugenzi mkuu yamedidimia. Batuli hajasita kwa uovu wake na ameshikana na Jojo kutimiza uovu wake! Dont miss it! Jumatatu hadi Jumatano saa 1 usiku!