Logo

Wiki hii katika MMBongo!

Habari
22 Januari 2018
Vipindi vya MMBongo ni via asili yetu hapa Tanzania, simulizi za maisha yetu na tamaduni zetu. Huu ndio uzuri wa MMBongo! Basi tujue yajayo!
MMB LOGO

Karibuni wapendwa kwa wiki nyingine hapa Maisha Magic Bongo! Kama mujuavyo, tumewaandalia burudani halisi na ya kufaa mahitaji yenu!

Vipindi vya MMBongo ni via asili yetu hapa Tanzania, ni simulizi za maisha yetu na tamaduni zetu. Huu ndio uzuri wa MMBongo! Basi tujue yajayo!

 

JUMATATU 22 JANUARI 2018:

SAKATA LA NDOA: 

Katika panda shuka za maisha haswa katika maisha ya ndoa, kunayo changamoto kadha wa kadha yanayowakumba wanandoa. Ni nini kinacho shikilia familia zetu? Tazama hadithi ya Mchungangaji pamoja na wafuasi wake na pilka pilka za maisha yao!

KAPUNI:

Huku mtaa wa pili mambo yanazidi kupamaba moto, wakati kila mmoja akitapatapa na huba lake usikose muendelezo wa tamthilia hii kila Jumatatu na Jumanne saa1;30 Usiku.

 

JUMANNE 23 JANUARI 2018:

MWANTUMU: 

Visa, visanga via Bwana Kaboba na marafiki wake kila Jumanne saa 1.30 usiku! Tazama highlights za kipindi hiki kila Jumatano katika mitandao yetu ya jamii (facebook, Twitter, instagram na Youtube)

BONGO FILAMU: 

Filamu mpya hapa #MMBongo kila siku saa 8 mchana au saa 2 usiku! Leo, filamu iitwayo Maumivu itakuwa hewani!

JUMATANO 24 JANUARI 2018:

SARAFU:

Baada ya binti yake Eng. Sanga kumwaibisha baba yake hadharani na kupokea rushwa kutoka Eng. Samwel ni nini kitakachofuata? Janeth na Mkewe Eng.Samwel katika sherehe moja, Damien naye, hasira zikimlenga moyo! Usikose kipindi cha leo saa 1.30 usiku!

 

ALHAMISI 25 JANUARI 2018;

DOLI ARMANO KI:

Changamoto za Urmi zimeanza kupunguka wakati alikata shauri kupambana na mume wake kwa kutumia mbinu za sheria! Usipitwe kila Alhamisi saa 12 jioni! 

MCHIKICHO WA PWANI:

Bi Mariam wa Migomba na mawaidha mufti ya kijamii akiguzia mada tofauti za kuimarisha maisha ya ndoa na nyumbani!

 

 

IJUMAA 26 JANUARI 2018:

MZOOKA:

Malizia wiki na tafrija ya Muziki moto moto kutoka Tanzania. Mzooka ni chemi chemi ya video mpya za Bongo fleva! Jumatatu hadi Ijumaa saa 10 jioni hapa #MMBongo!

KITIMTIM: 

Bwana Mbote na mke wake wanarejea kuleta vichekesho bila kifani! Kila jumma saa 1 usiku hapa #MMBongo!