Logo

Yajayo katika MMBongo wiki hii!

Habari
30 Julai 2018
Vipindi vipya, tamthilia za kipekee na mengineo! SOMA HAPA!
<p>Screen Shot 2018-07-30 at 16.27.18</p>

 

Wiki iliyopita, tulishuhudia mwanzo wa vipindi vipya hapa Maisha Magic Bongo. Msimu wa tatu wa Harusi Yetu uliendelea na ndoa kati ya Mary na Daniel, wapenzi wa zamani waliokutana katika chou kikuu, UDOM. Camera zetu zilifuatana nao kwa kila hatua na kutuleta kipindi moto moto kila Alhamisi saa 1 usiku!

 

Tamthilia ya kipekee, BLOOD imepeperushwa katika runinga zetu na masaibu ya Stacey yanaendelea kuchacha! Kipindi cha kusisimua Jumanne na Jumatano saa …USIKOSE!

Kulingana na matakwa ya watazamaji wetu, tumewaandalia kipindi kipya cha KUMI ZA WIKI! Muziki wetu bora zilizochaguliwa ni wewe mtazamaji, zinaorodheshwa katika kipindi hiki. Kila Ijumaa saa 11 jioni! Tarajia filamu mpya za mwisho wa wiki. Kila Jumanne hadi Alhamisi saa 8 mchana, filamu za #MMBongo