Logo
Mengine Zaidi
channel logo dark

Pazia

160TamthiliaPG13

Yaliyomo katika ulimwengu wa burudani

Habari
19 Februari 2018
Pata kionjo cha pilka pilka za ulimwengu wa sanaa na burudani!
SteveNyerere

 Katika mwezi huu wa Februari, kuna mabadiliko mengi yanayofanyika hapa nchini Tanzania, Afrika Mashariki na katika bara la Afrika kwa jumla. 

Waafrika wametimiza wakati ambapo wanamatumaini na hisia za maendeleo katika bara letu. Watu wetu wanasherehekea uzuri wa nchi zetu na tamaduni zetu tofauti kote Afrika.

Hapa nyumbani, tarehe 10 Februari,  tuliungana na mwana muziki mashuhuri Ambwene Yessiah (A.Y) tukimpongeza kwa kumposa na kumwoa binti kutoka nchi ya Rwanda!  A.Y na Remy walifunga ndoa ya kitamaduni katika shughuli ya kijamii na marafiki wa karibu, mjini Kigali. Hongera kwa maharusi hawa!

 

Katika mitandao ya kijamii ya Maisha Magic Bongo,mashabik na watazamaji wetu walifurahi sana kutazama vipindi vya #MMBKapuni!

 

Tukivuka kwenye sekta ya sanaa ya sinema, filamu mashuhuri kote duniani, ‘Black Panther’ ilionyeshwa katika sinema za Tanzania na bara la Afrika kwa jumla. Mashabik wa filamu walijitokeza kusherehekea filamu iliyofuata mitindo na maudhui ya kiafrika.

Vile vile, hapa nyumbani, msanii kikongwe Steve Nyerere alilalamika na kusema sekta ya uaandaji wa filamu hawatoi nafasi kwa wasanii wadogo wadogo katika uzalishaji wa filamu. Ni shida kupata wasanii wale wale wakiigiza katika filamu zote.

Kwa sekta ya muziki, Diamond na mke wake Zari bado wako katika changamoto za kindoa. Siku ya mapenzi (February 14) Zari alisemekana kusema kwamba hana haja na mahusiano na mume wake. Diamond bado hajatoa taarifa kamili na tunawaombea kila la kheri.

Pata filamu za Bongo hapa wiki hii tukikamilisha mwezi Februari movies! Maisha Magic Bongo ni mambo yote! Ungana nasi!