Habari za ulimwengu wa sanaa na filamu mwezi wa Mei!

Yaliyo katika Sanaa na filamu hapa #MMBongo!

08 Mei 2018

Katika habari za Sanaa zetu, msanii maarufu Mbosso aliyesajiliwa na WCB nyota yake inangaa! Na ndani ya kipindi hichi kifupi ameachia ngoma mfululizo na zote zinafanya vizuri sana. Hivi sasa, ana wimbo mpya, ‘Alele’

1525791238 34 screen shot 2018 05 07 at 12.05.45

Kwa ulimwengu wa filamu za Bongo, Daudi Micheal  (Duma) amejitolea kuimarisha sekta ya Sanaa katika filamu. Amelenga macho na kuvuka mipaka ya Afrika kuungana na wazalishaji maarafu kutoka ngambo kwa aajili ya kushirikiana katika mengi yatakayo saidia kukuza Sanaa uendeshaji na  uuzaji ya filamu za kiTanzania duniani .

1525791333 34 duma

Yvonne Cherrie Monalisa amepaa kama muigizaji wa kike bora hapa Tanzania! Ameibuka msanii bora wa kike katika tuzo za African Prestigious Awards (APA), Tunasherehekea naye na kumtakia kila la kheri! Na aendele kuipeperusha bendera ya Tanzania kote ulimwenguni!

1525791381 34 yvonne cherrie monalisa

Ungana nasi wiki hii!