Mwongozo wa kutuma mawasilisho ya AMVCA 2018.

28 Aprili 2018

 

Mashindano ya AMVCA 2018 yatakuwa tarehe 1 Septemba mwaka huu wa 2018.  Hakikisha umetuma wasilisho lako kabla ya tarehe 30 Aprili 2018.

 

Mashindano ya AMVCA 2018 yatakuwa tarehe 1 Septemba mwaka huu wa 2018.  Hakikisha umetuma wasilisho lako kabla ya tarehe 30 Aprili 2018.

Hatua ya 1:

Tayarisha video ya dakika mbili au tatu itakayokuwa wasilisho lako la mtandao wa intaneti. Tafadhli hakikisha video yako itaonyesha maudhui yatakayo sisitizwa katika kategori unayopendekeza kazi yako. Pia, hakikisha video yako haijapitisha muda uliosisitizwa na faili haijazidisha 500mb.

 

Hatua ya 2: 

Video yako ikiwa tayari, tembelea ukurasa wa mawasilisho: www.amvca2018.com/submit. Utahitaji kujaza fomu na maelezo ya kibinafsi kama jina, nchi, nambari ya passpoti, kwa hivyo, hakikisha uko na ujumbe huu tayari. Ukimaliza kujaza fomu, bonyeza "SUBMIT". Baada ya kutuma wasilisho, utapata nambari ya kipekee (unique reference number). Weka nambari hii kwa matumizi baadaye. 

 

Hatua ya 3:

Ukikosa kufaulu kutuma wasilisho lako katika mtandao wa submissions, tafahdhali rekodi video yako katika CD au flash disk/drive na kuipeleka wewe binafsi katika anwani zifuatazo: (Hakikisha umeandika nambari yako ya kipekee - unique reference number)

Attention: Hadizat Ibrahim (Nigeria)

Mss Local Productions

4 industrial street, off town planning way,

Illupeju, Lagos

Nigeria

 

Attention: Buhle Ngcauzele (South Africa)

137 Bram Fischer Drive,

Randburg, 2123,

South Africa.

 

Attention: Margaret Mathore (Kenya)

2nd floor, M-Net Offices

Local Production studio,

Jamhuri Grounds off Ngong Road,

Nairobi,

Kenya.

Tafadhali hakikisha umetuma wasilisho lako kabla ya Jumatatu, 30 Aprili 2018 saa 5.59 usiku. Tunawatakia kila la kheri. 

Msimu wa sita (6) wa AMVCA unaletwa kwako ni Konga, Nokia Phones na Heritage Bank. Ungana nasi katika kurasa zetu za kijamii  Facebook,   Twitter & Instagram kwa maelezo zaidi kuhusu shindano hili.