Logo
Mwantumu Slim
channel logo dark

Mwantumu

160ComedyPG13

Habari kutoka MWANTUMU: Mchekeshaji Lucas Mhuvile a.k.a JOTI

Habari
09 Novemba 2017
Tukiendelea na taswira yetu ya MOVEMBER mwezi huu wa Novemba, tungependa kuwashukuru wanaume waliopaa katika sekta ya burudani ya Filamu, Muziki na Televisheni!
Instagram

Tukiendelea na taswira yetu ya MOVEMBER mwezi huu wa Novemba, tungependa kuwashukuru wanaume waliopaa katika sekta ya burudani ya Filamu, Muziki na Televisheni! Wiki hii, tunarusha macho katika kipengele cha Vichekesho au Comedy katika sekta ya burudani ya Televisheni.

Hapa Maisha Magic Bongo, tuna hisia za kuwajulisha wote, haswa wanaume umuhimu wa kushirikiana na madaktari kupata ujuzi zaidi kuhusu Kansa ya sehemu Nyeti. Pia, magonjwa ya saikolojia katika wanaume ambayo hayatiliwi maanani katika jumuiya zetu na kwa mara nyingi, watu ambao wanaweza kupata matibabu, wanatupiliwa mbali. 

Leo, tunalenga macho kwa muigizaji kikongwe, Bw. Lucas Lazaro Mhuvile ajulikanaye kama Joti. Lucas Lazaro alizaliwa 9 Julai 1982 katika mkoa wa Morogoro, wilaya ya Ulanga.  Sanaa ya Lucas ilianza akiwa bado mtoto akiwa mchekesahji maarafu katika vikundi vya uigizaji shuleni. Aliendelea kujiunga na vikundi mbali mbali kuijenga talanta yake. Kutoka mwaka wa 2000, Joti alichezea vikundi tofauti kama Sunrise, Nyota Ensemble na hatimaye, Ze Comedi.

Baada ya mwaka 2003, Joti alihamisha usanii wake kwenye Televisheni na kushirikiana na wasanii wachekeshaji kutoka Afrika Mashariki. Kwa sasa, Joti anaigiza kipindi kipya katika chaneli ya MAISHA MAGIC BONGO  katika kifurushi cha DSTv kiitwacho MWANTUMU. Katika kipindi hiki, Lucas anaigiza kama kijana mwerevu, mkimbiza-rinda anayejaribu kujitafutia riziki lakini, utukutu wake unamtia katika changamoto nyingi! 

Usikose kipindi cha #MwantumuTZ kila Jumanne saa 1.30 usiku kupitia Maisha Magic Bongo katika DStv chaneli 160! Ni yetu! 

Kupata habari zaidi, temebelea kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na tovuti yetu: maishamagicbongo.tv